Rapa kutoka Nigeria Olamide anatarajia kutoa album yake ya tano “Eyan Mayweather” November 23 2015.
Olamide hajaoa album toka mwaka 2011,amesema album yake mpya itaitwa “Eyan Mayweather” na itakuwa na nyimbo 20, nyimbo kama Bobo,Matters Arising,Melo melo na Lagos Boys zipo.
Olamide pia ameweka wazi kuwa hakuna collabo yeyote kwenye album hii na kwamba kila kitu kafanya yeye.
Mwanzoni mwa mwaka huu Olamide na rapa Phyno walitoa album ya pamoja iliyoitwa “2 Kings”.
Hivi karibuni Olamide alishinda tuzo ya Best Male Artiste In West Africa kwenye tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA).




